Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hafla ya ufunguzi wa Hawza hiyo imefanyika siku ya Jumapili, tarehe 1 Novemba 2026, ikiwa ni hatua muhimu katika juhudi za kuimarisha elimu ya dini, malezi ya kiroho na makuzi ya kimaadili miongoni mwa vijana wa Kiislamu katika eneo hilo.
Hawza hiyo imetambulika kwa jina la Hawza Imam Zaynul Abidina (as), ikiwa na lengo la kuwa kituo cha kielimu na kimalezi kitakachochangia kuwajenga vijana katika misingi sahihi ya mafundisho ya Ahlulbayt (as), kuwalea kwa maadili mema na kuwaandaa kuwa watu wenye uelewa wa dini yao pamoja na kuwajibika katika jamii.
Hawza hiyo itakuwa chini ya usimamizi wa Sheikh Husein Seif Kaduguda, ambaye ni mas’uli mkuu wa Hawza hiyo.
Ufunguzi wa taasisi hii ya kielimu ni hatua inayodhihirisha dhamira ya uongozi wa Markaz Kunuuzil Jannah katika kuwekeza katika elimu na malezi ya kizazi kipya, kwa kutambua umuhimu wa kuwajenga vijana wenye elimu, maadili na mwenendo unaozingatia mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Hatua hii pia inatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha shughuli za kielimu na kimalezi katika Kijiji cha Kazole na maeneo ya jirani, huku ikitoa fursa kwa vijana wa Kiislamu kupata elimu ya dini katika mazingira yanayowajali na kuwajenga kiroho na kimaadili.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aibariki Hawza Imam Zaynul Abidina (as), awape tawfiki viongozi na walimu wake katika kutekeleza majukumu yao, na aijaalie kuwa chimbuko la wanazuoni, waelimishaji na vijana wenye maadili mema watakaolitumikia dini na jamii.




Maoni yako